COMHESWA TALKS

COMHESWA TALKS

COMHESWA TALKS ni jukwaa la mazungumzo na mahojiano linaloandaliwa na COMHESWA kwa lengo la kuelimisha, kuhamasisha, na kuibua mijadala yenye kujenga kuhusu maendeleo ya jamii. Lengo letu ni kushiriki maarifa, uzoefu, na suluhisho zinazoweza kuwahamasisha watu binafsi na jamii kuchukua hatua kuelekea mabadiliko chanya na maendeleo endelevu.

Jiunge nasi katika kila kipindi, usisahau Subscribe, bonyeza Like, toa maoni yako, na share video hizi ili ujumbe wa mabadiliko uwafikie watu wengi zaidi. COMHESWA TALKS – Sauti ya Maarifa, Chanzo cha Mabadiliko.

MAFUNZO, USHONAJI NA UTHUBUTU

Huyu ni Mnufaika wa Mafunzo Amali na Ujasiriamali kutoka COMHESWA, aliyebadili maisha yake kupitia ujuzi wa ufundi, elimu ya ujasiriamali, na uthubutu wa kuanzisha biashara ya ushonaji nguo.

JINSIA, MALEZI NA JAMII

Je, usawa wa kijinsia ni suala linalowahusu wanawake pekee? Je, mwanaume ana nafasi gani katika kujenga jamii yenye usawa? Na kwa nini bado kuna vitendo vingi vya ukosefu wa usawa ambavyo jamii imevichukulia kuwa vya kawaida? Jifunze kutoka kwa Mtaalamu wa Masuala ya Jinsia wa COMHESWA.

SAFARI YA COMHESWA

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la COMHESWA na Kampuni ya COMHESWA PLUS COMPANY LIMITED akielezea kwa undani historia ya COMHESWA, sababu zilizopelekea kuanzishwa kwake, changamoto za kijamii ilizolenga kutatua, pamoja na safari ya kujenga taasisi yenye lengo la kuleta mabadiliko chanya katika jamii.